| Mea wa jiji la Arusha Calist Lazarro |
Amesema kuwa sheria ya mwaka 2016 iliyowekwa na wabunge hivi karibuni imemkandamiza Mwandishi wa Habari kwani inamtaka awe na kiwango cha elimu ya Shahada ndipo atambulike kama mwanahabari, ivyo wanaotunga sheria hizo ni wabunge ivyo nao wawe na Elimu yakutosha wawapo Bungeni.
Aidha Lazarro alitoa rai kwa waandishi wa habari waliohitimu pamoja na walioko katika vyombo vya habari kuwa wazitumie kalamu zao kuwatetea wanyonge pamoja na kufanya kazi katika maadili ili kuepukana na kesi za kuvunja sheria mpya zilizowekwa na wabunge hivi karibuni
![]() |
| Wahiti wa Arusha journalism Training College |
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi waliohitimu hapo jana Bwana Underson Bugoma amesema anamshukuru mungu kwa kumjalia kuhitimu masomo yake salama na kuhaidi atakuwa mwandishi makini na kusimamia ukweli na si kinyume na hapo...

Aidha mmoja wa wanafunzi anayesalia chuoni hapo Bi Asha Kabuga ameeleza kusikitishwa na kuhitimu kwa wanafunzi hao lakini ameeleza kuwa pamoja na kuwapenda na kuwazoea wao bado watawahitaji ili kufika mbali zaidi katika tasnia.

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ni miongoni wa vyuo ambavyo vinatoa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji nchini na kinashika nafasi ya pili Tanzania kwa mujibu wa NACTE.

No comments:
Post a Comment